Monday, December 31, 2007

HERI ZA MWAKA MPYA 2008

KWA NIABA YA WATANZANIA WAISHIO TAMPERE, NAPENDA KUWATAKIA WADAU WOTE WA BLOG HII HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA 2008!

Wednesday, December 26, 2007

KRISMASI YA 2007

Mwaka huu sikukuu ya Krismasi ilisherehekewa kwa ujumla nyumbani kwa Dr. Augustino Binamu ambapo wadau wengi walihudhuria. Picha zitajieleza zenyewe!


Dr. Augustino Binamu (kulia)

Monday, December 10, 2007

SHULE ZA TAMPERE

Hapa Tampere kuna shule nyingi ambazo zinatoa mafunzo mbalimbali. Hapa ni kwenye shule ambayo inafundisha vijana waliohitimu mafunzo ya sekondari kujofunza umekanika wa ndege. Finland kuna nafasi nyingi sana za masomo, na hivi karibuni vijana wengi wa ki Tanzania wamekuwa wakichangamkia nafasi hizo. Kitu kizuri zaidi ni kuwa hakuna gharama zozote za ada!

Tuesday, December 4, 2007

MGENI KUTOKA MWANZA

Pichani ni Mwalimu WINFRIDA MASANJA kutoka shule ya Igoma, Mwanza, ambaye kwa sasa yupo Tampere kutembelea shule za hapa mjini katika mpango maalum wa urafiki kati ya mji wa Mwanza na Tampere.