Monday, December 31, 2007

HERI ZA MWAKA MPYA 2008

KWA NIABA YA WATANZANIA WAISHIO TAMPERE, NAPENDA KUWATAKIA WADAU WOTE WA BLOG HII HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA 2008!

Wednesday, December 26, 2007

KRISMASI YA 2007

Mwaka huu sikukuu ya Krismasi ilisherehekewa kwa ujumla nyumbani kwa Dr. Augustino Binamu ambapo wadau wengi walihudhuria. Picha zitajieleza zenyewe!


Dr. Augustino Binamu (kulia)

Monday, December 10, 2007

SHULE ZA TAMPERE

Hapa Tampere kuna shule nyingi ambazo zinatoa mafunzo mbalimbali. Hapa ni kwenye shule ambayo inafundisha vijana waliohitimu mafunzo ya sekondari kujofunza umekanika wa ndege. Finland kuna nafasi nyingi sana za masomo, na hivi karibuni vijana wengi wa ki Tanzania wamekuwa wakichangamkia nafasi hizo. Kitu kizuri zaidi ni kuwa hakuna gharama zozote za ada!

Tuesday, December 4, 2007

MGENI KUTOKA MWANZA

Pichani ni Mwalimu WINFRIDA MASANJA kutoka shule ya Igoma, Mwanza, ambaye kwa sasa yupo Tampere kutembelea shule za hapa mjini katika mpango maalum wa urafiki kati ya mji wa Mwanza na Tampere.

Wednesday, November 28, 2007

MENARD MPONDA, U WAPI?

Naitwa Alex Rwambali nipo GERMANY; tafadhali naomba contact za MEDAD MPONDA huyo jamaa tulikuwa nae pale Bagamoyo miaka ya 1993-1995 alinitangulia mwaka mmoja. Email yangu hiyo hapo.Nashukuru in advance
amagere@hotmail.com

November 27, 2007 5:30 PM

USIKU WA MWAFRIKA, JOENSUU

Naitwa Sunday Ngakama toka Mwanza, ninapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio Finland kwamba kutakuwa na usiku wa Mwafrika tarehe 28 Novemba, katika ukumbi wa jiji la Joensuu, Teatteri Klubi.

Kwa maelezo zaidi, mawasiliano kwa: sundayngakama@yahoo.co.uk, au 0505373949. Asanteni!

Sunday, November 18, 2007

MWANZA NITE

Hapo jana, tarehe 17 Novemba 2007 katika ukumbi wa KLUBI kulikuwa na sherehe za kuadhimisha Mwanza Day. Sherehe hizo zilifanikishwa na muziki wa disko (ngwasuma, bongo flava n.k.) uliopigwa na DJ George Matovu, nyimbo na ngoma za vijana wa Mponda (hatuondoki mpaka pombe iishe) , ngoma na muziki wa kantele ulipigwa pia na kikundi cha Bandu Bandu kikiongozwa na Arnold Chiwalala. Vijana wa Cheza ngoma walifurahisha watazamaji kwa ngoma zao mbalimbali, hasa ile ya gobogobo. Bendi ya Galaxy (wanamuziki wa Senegali) kutoka Helsinki walifurahisha pia watazamaji kwa muziki wao wa Senegal hasa kutokana na ile ngoma yao inayoteta.

George Matovu


Mpondas


Bandu Bandu


Galaxy on stage



Klubi

Wageni kutoka Mwanza






Sunday, November 11, 2007

GRADUATION PARTY YA ROBERT MHEKWA

Tarehe 10 Novemba 2007, siku ya Jumamosi tulijumuika pamoja kusherehekea graduation ya ndugu yetu Robert Mhekwa pale alipochukua nondoz zake. Picha zenyewe zinajieleza.


Robert Mhekwa (kushoto)



Tuesday, October 16, 2007

AUTUMN IMEWADIA

Kipindi cha autumn kimewadia kwetu. Katika kipindi hiki, baridi huanza kuwa kali, majani hupukutika kutoka mitini na jua linachelewa kuchomoza asubuhi, na kuzama wakati wa adhuhuri. Matokeo yake ni kuwa katika giza kwa muda mrefu zaidi. Ili kuchangamsha nafsi za watu, kunakuwa na mapambo ya taa katika barabara kubwa ya Tampere, Hameenkatu.

Hameenkatu leo saa 5 asubuhi (16/10/2007)

Saturday, September 29, 2007

MNADA WA POLISI

Leo kuanzia saa sita mchana palikuwepo na mnada wa Polisi ambapo vitu vingi vilinadiwa. Vitu hivyo vilikuwa baiskeli, navigators, playstation, simu na kadhalika. Mnada kama huu hufanyika kila mwaka wakati kama huu na unaweza kujipatia kifaa kizuri kwa bei ya mnadani. Niliona wanafunzi Wachina na Wahindi ambao walinunua baiskeli.

Thursday, September 27, 2007

Monday, September 24, 2007

KARIBUNI

Karibuni katika blog hii kutoa maoni, matangazo kuweka picha na kadhalika.