Tuesday, October 16, 2007

AUTUMN IMEWADIA

Kipindi cha autumn kimewadia kwetu. Katika kipindi hiki, baridi huanza kuwa kali, majani hupukutika kutoka mitini na jua linachelewa kuchomoza asubuhi, na kuzama wakati wa adhuhuri. Matokeo yake ni kuwa katika giza kwa muda mrefu zaidi. Ili kuchangamsha nafsi za watu, kunakuwa na mapambo ya taa katika barabara kubwa ya Tampere, Hameenkatu.

Hameenkatu leo saa 5 asubuhi (16/10/2007)

1 comment:

Ndaki said...

Hakika kazi nzuri ya kutuletea jinsi majira ynavyopokezana "vijiti".

Na nikipindi ambacho kwa sisi wapenzi wa viumbe hai kama ndege basi ndio wanakuwa wakituimbia nyimbo za kwaheri wakielekea kwenye hali ya hewa ya joto.Wazalendo walinihabarisha wanaenda Spain bila visa(lol).