Wednesday, November 28, 2007

MENARD MPONDA, U WAPI?

Naitwa Alex Rwambali nipo GERMANY; tafadhali naomba contact za MEDAD MPONDA huyo jamaa tulikuwa nae pale Bagamoyo miaka ya 1993-1995 alinitangulia mwaka mmoja. Email yangu hiyo hapo.Nashukuru in advance
amagere@hotmail.com

November 27, 2007 5:30 PM

USIKU WA MWAFRIKA, JOENSUU

Naitwa Sunday Ngakama toka Mwanza, ninapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio Finland kwamba kutakuwa na usiku wa Mwafrika tarehe 28 Novemba, katika ukumbi wa jiji la Joensuu, Teatteri Klubi.

Kwa maelezo zaidi, mawasiliano kwa: sundayngakama@yahoo.co.uk, au 0505373949. Asanteni!

Sunday, November 18, 2007

MWANZA NITE

Hapo jana, tarehe 17 Novemba 2007 katika ukumbi wa KLUBI kulikuwa na sherehe za kuadhimisha Mwanza Day. Sherehe hizo zilifanikishwa na muziki wa disko (ngwasuma, bongo flava n.k.) uliopigwa na DJ George Matovu, nyimbo na ngoma za vijana wa Mponda (hatuondoki mpaka pombe iishe) , ngoma na muziki wa kantele ulipigwa pia na kikundi cha Bandu Bandu kikiongozwa na Arnold Chiwalala. Vijana wa Cheza ngoma walifurahisha watazamaji kwa ngoma zao mbalimbali, hasa ile ya gobogobo. Bendi ya Galaxy (wanamuziki wa Senegali) kutoka Helsinki walifurahisha pia watazamaji kwa muziki wao wa Senegal hasa kutokana na ile ngoma yao inayoteta.

George Matovu


Mpondas


Bandu Bandu


Galaxy on stageKlubi

Wageni kutoka Mwanza


Sunday, November 11, 2007

GRADUATION PARTY YA ROBERT MHEKWA

Tarehe 10 Novemba 2007, siku ya Jumamosi tulijumuika pamoja kusherehekea graduation ya ndugu yetu Robert Mhekwa pale alipochukua nondoz zake. Picha zenyewe zinajieleza.


Robert Mhekwa (kushoto)