Friday, January 11, 2008

FILOSOFIA

Nimeshasoma maneno mengi yaliyojaa filosofia nzuri, na natumaini wengi wenu mmeshayasoma pia. Kuna nmaneno fulani niliyaona yamebandikwa kwenye ukuta wa sebule wa nyumba moja hapa Tampere, ambayo yalinifanya nitafakari sana. Labda na wewe yatakufanya utafakari. Maneno yenyewe yalikuwa katika lugha ya kiingereza, na yalikuwa kama yafuatavyo:

"ALL VISITORS WHO COME TO THIS HOUSE MAKE US VERY HAPPY, SOME WHEN THEY ARRIVE AND SOME WHEN THEY LEAVE"

Upo hapo?

Na katika pitapita zangu leo katika mitaa ya Tampere niliona jamaa kaandika haya maandishi katika mojawapo ya mabin ya mjini. Nikafikiria ni kitu gani kilichomfanya jamaa huyu kuandika haya maneno, tena kwa ufanisi mzuri. Nikatafakari, nikasema; "Mmhhh". Wewe je?
No comments: