

Nakumbuka nilipokuwa mdogo, baba yangu alikuwa na pickup ya Peugeout, wakati huo tulikuwa tunayaita Pijo. Hayo magari yalikuwa maarufu sana na yalikuwa yanafanya kazi nyingi sana, kama magari ya kawaida ya nyumbani, kubebea mizigo na hata kama taxi. Baadae miaka ya 1980 magari hayo yalivuma sana sifa, zilipoingizwa Tanzania kwa wingi Peugeout 504 ambazo zilijulikana kama Guruwe. Nimepata fursa ya kupiga picha baadhi ya Peugeot za zamani: