Friday, August 7, 2009

Magari ya PeugeotNakumbuka nilipokuwa mdogo, baba yangu alikuwa na pickup ya Peugeout, wakati huo tulikuwa tunayaita Pijo. Hayo magari yalikuwa maarufu sana na yalikuwa yanafanya kazi nyingi sana, kama magari ya kawaida ya nyumbani, kubebea mizigo na hata kama taxi. Baadae miaka ya 1980 magari hayo yalivuma sana sifa, zilipoingizwa Tanzania kwa wingi Peugeout 504 ambazo zilijulikana kama Guruwe. Nimepata fursa ya kupiga picha baadhi ya Peugeot za zamani:

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimekukuta kwa kaka Simon Kitururu nikaona si vibaya kukutaka hali.

Tanzania Safari said...

Nimependa sana Blog yako. Nzuri sana. Jamani endeeleni kutangaza Nchi yetu ya Tanzania hata munapokuwa Ng'ambo. Msii ponde nchi yetu bali tangazeni uzuri uliopo.