Monday, November 23, 2009


Peugeuot

Really?

Footprints on snow

Really, made in Russia

Friday, August 7, 2009

Magari ya Peugeot



Nakumbuka nilipokuwa mdogo, baba yangu alikuwa na pickup ya Peugeout, wakati huo tulikuwa tunayaita Pijo. Hayo magari yalikuwa maarufu sana na yalikuwa yanafanya kazi nyingi sana, kama magari ya kawaida ya nyumbani, kubebea mizigo na hata kama taxi. Baadae miaka ya 1980 magari hayo yalivuma sana sifa, zilipoingizwa Tanzania kwa wingi Peugeout 504 ambazo zilijulikana kama Guruwe. Nimepata fursa ya kupiga picha baadhi ya Peugeot za zamani:

Label ya kutoka Tanzania

Juzi nilipitia kwenye duka la Lidl kutafuta bidhaa mbalimbali, zikiwemo na chakula. Katika kupitia mashelf mbalimbali nikaona hii T shirt yenye label ya Serengeti. Nikafurahi kuona jina la nyumbani, na nikahisi labda imetoka kwetu nyumbani . Kuichunguza kwa karibu nikaona kuwa imetengenezwa Ujerumani. Sijui sana mambo ya kisheria, hivyo nikabaki nimeduwaa, je ni vipi hawa jamaa kutumia majina yetu, ni sawa?

Monday, October 27, 2008

Sunday, June 1, 2008

SUMMER IMEINGIA

Summer (kipindi cha joto) imeanza na kama ilivyo kawaida ya huku, ni wakati wa kufurahia maisha ya nje baada ya kipindi kirefu cha baridi, ambacho inabidi kwa wakati mwingi, watu wakae ndani. Hivyo basi wakati wa joto shughuli nyingi hufanywa nje na kuendelea kwa muda mrefu kwa kuwa jua halizami katika kipindi hiki.

Hapo chini ni katika Grill Party aliyoifanya Menard Mponda na kuwaalika rafiki zake, wa Tanzania na kutoka nchi zingine mbalimbali.










Sunday, March 23, 2008

EASTER


Hapa Tampere Pasaka ilifana kwa jamii ya Watanzania na rafiki zao, ambapo matukio mbalimbali yalifanyika ya kusherehekea pamoja.

Monday, February 11, 2008

FEST AFRICA 2008

FEST AFRICA 2008


DEAR FRIENDS
FEST AFRIKA PRESENTS AN AFRICAN WINTER JAM FESTIVAL. SPICED WITH LOTS OF HAPPENINGS AND GREAT LIVE EVENTS. ATTACHED BELOW IS THE PROGRAMME, PLEASE GO THROUGH IT. COME ONE COME ALL. TICKETS ON SALE IN ADVANCE (check below), PLEASE HURRY AND DON'T MISS A CHANCE TO PARTICIPATE IN THE BEST AFRICAN EVENT OF THE YEAR. PLEASE FORWARD TO FRIENDS.


DATE : SATURDAY 23.02.2008
TIME : 20-04:00
PLACE: KLUBI-TAMPERE-FINLAND


SUPPORTING ARTISTS :-

.PAPA ZAI-FROM ZAMBIA - ROOTS REGGAE SOUND SYSTEAM.
.CHEZA NGOMA - Fin -Tanzania-Afro dance.
.SAMBA GIRLS -Fin-
Oba oba.
.
OCG-Tanzania
RnB and HipHop.
.MPONDA´S-
Singing, drumming and body movements.

MAIN BAND


.PABLOMACHINE and THE TANGANYIKA SOUND- From Tanzania & Burundi (based in Sweden)

Plays Ndombolo, Afro-Rumba, Soukous, Afro-Beats & much more


DJs CLIFF (dj hakuna matata)
Fidelis- Sweden
Mambo Team


TICKETS 10€ Advance at Klubi, Epe´s and Swamp Music;
15€ at the door


Links:

www.festafrika.net
www.pablomachine.podomatic.com
www.bredband.net
www.chezangoma.net

Friday, January 18, 2008

JETFIGHTER


Unaweza kujifunza kuwa fundi wa jetfighter!

Friday, January 11, 2008

CATHEDRAL LA TAMPERE

FILOSOFIA

Nimeshasoma maneno mengi yaliyojaa filosofia nzuri, na natumaini wengi wenu mmeshayasoma pia. Kuna nmaneno fulani niliyaona yamebandikwa kwenye ukuta wa sebule wa nyumba moja hapa Tampere, ambayo yalinifanya nitafakari sana. Labda na wewe yatakufanya utafakari. Maneno yenyewe yalikuwa katika lugha ya kiingereza, na yalikuwa kama yafuatavyo:

"ALL VISITORS WHO COME TO THIS HOUSE MAKE US VERY HAPPY, SOME WHEN THEY ARRIVE AND SOME WHEN THEY LEAVE"

Upo hapo?

Na katika pitapita zangu leo katika mitaa ya Tampere niliona jamaa kaandika haya maandishi katika mojawapo ya mabin ya mjini. Nikafikiria ni kitu gani kilichomfanya jamaa huyu kuandika haya maneno, tena kwa ufanisi mzuri. Nikatafakari, nikasema; "Mmhhh". Wewe je?




Monday, December 31, 2007

HERI ZA MWAKA MPYA 2008

KWA NIABA YA WATANZANIA WAISHIO TAMPERE, NAPENDA KUWATAKIA WADAU WOTE WA BLOG HII HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA 2008!

Wednesday, December 26, 2007

KRISMASI YA 2007

Mwaka huu sikukuu ya Krismasi ilisherehekewa kwa ujumla nyumbani kwa Dr. Augustino Binamu ambapo wadau wengi walihudhuria. Picha zitajieleza zenyewe!


Dr. Augustino Binamu (kulia)

Monday, December 10, 2007

SHULE ZA TAMPERE

Hapa Tampere kuna shule nyingi ambazo zinatoa mafunzo mbalimbali. Hapa ni kwenye shule ambayo inafundisha vijana waliohitimu mafunzo ya sekondari kujofunza umekanika wa ndege. Finland kuna nafasi nyingi sana za masomo, na hivi karibuni vijana wengi wa ki Tanzania wamekuwa wakichangamkia nafasi hizo. Kitu kizuri zaidi ni kuwa hakuna gharama zozote za ada!

Tuesday, December 4, 2007

MGENI KUTOKA MWANZA

Pichani ni Mwalimu WINFRIDA MASANJA kutoka shule ya Igoma, Mwanza, ambaye kwa sasa yupo Tampere kutembelea shule za hapa mjini katika mpango maalum wa urafiki kati ya mji wa Mwanza na Tampere.

Wednesday, November 28, 2007

MENARD MPONDA, U WAPI?

Naitwa Alex Rwambali nipo GERMANY; tafadhali naomba contact za MEDAD MPONDA huyo jamaa tulikuwa nae pale Bagamoyo miaka ya 1993-1995 alinitangulia mwaka mmoja. Email yangu hiyo hapo.Nashukuru in advance
amagere@hotmail.com

November 27, 2007 5:30 PM